info@abcpswahili.co.tz
(+255)712 029 665

Nani muhusika nyuma ya pazia?

Wahusika

Utafiti unaonyesha kuwa kila mwaka kiasi cha dola za Marekani bilioni moja ikiwa sawa na zaidi ya fedha za kitanzania Tshs trilioni 2.25 zinapotea kila mwaka kutokana na kupungua kwa mazao ya misitu, uvuvi na wanyama pori. Pia inaonesha kuwa ukame wa mwaka 2003 ulisababisha kupungua kwa kiwango cha kukua kwa uchumi kwa asilimia 10. Matokeo ya tafiti hizo yanaashiria kuwa matatizo yatakuwa makubwa zaidi katika siku za baadaye endapo uharibifu wa mazingira hautapatiwa ufumbuzi hasa ukizingatia mabadiliko ya tabianchi kama vile maafa yaliyotokana na mafuriko yaliyotokea wakati wa El NiƱo na kuzama kwa kisiwa cha "Maziwe" ambacho kilikuwa mazalia ya kasa na samaki katika pwani ya Pangani mkoani Tanga. Kufikia hatua hii, watetezi wa mazingira wamefanya kazi ya kutosha, na taarifa zote hizi zitakuwa kazi bure kama hazitapewa kipaumbele na wanasiasa.

img
Kibosho

Kitabu cha Kibosho Mashariki

Jamii na vikundi vya mzaingira mbalimbali kutoka Kibosho mashariki na vile vilivyopo jirani na mlima mkoani Kilimanjaro Tanzania, kwasababu ya uthubutu wao na utayari walionao juu ya utunzaji wa mazingira, walipewa na kuchaguliwa kuwa mkoa pekee utakao fanya sherehe za mazingira ...

img
Wanawake

Vikundi vya Wanawake

Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi zaidi ya wanaume. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa asilimia 80 ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake Majukumu yao kama walezi na wanao hudumia familia....

img
Jamii

Vikundi vya Jamii

African blackwood conservation project (ABCP) ilianzishwa 1996 ikiwa na lengo la kuunganisha Jamii na mazingira yao. Huwa inashirikisha sana jamii kikamilifu kwani ni moja wapo kati ya maono yetu ni kuwa na watu wenye maono chanya juu ya utunzaji wa mazingira na kuwa na uelewa na kuyatunza....

img
Vikundi mashuleni

Vikundi Mashuleni

Shule bila elimu haiwezekani, na mazingira bila elimu ni mafanano wake. Kufanikisha uoteshaji wa miti na kurudisha uoto wa asili ni ngumu sana. Ila uwepo waelimu kwa kuwaelimisha watoto kwanzia ngazi ya chini ni rahisi sana kuepusha uharibifu na kurejesha hali chanya kwa mazingira ya baadae...