info@abcpswahili.co.tz
(+255)712 029 665

Kibosho Mashariki

Taarifa za kitafiti kutoka BBC zinaonyesha kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi zaidi ya wanaume. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa asilimia 80 ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake. Majukumu yao kama walezi na wanao hudumia familia kwa karibu zaidi huwafanya kuwa katika mazingira hatari zaidi wakati wa mafuriko na ukame unapotokea. Makubaliano ya mjini Paris mwaka 2015 yaliweka kipaumbele maalum cha uwawezesha na kutambua kwamba wanawake huathiriwa kwa kiasi kikubwa zaidi katika jamii utokana na mabadiliko ya tabia nchi. Afrika ya kati, eneo ambalo ziwa Chad limetoweka kwa asilimia 90, hali inayolazimu wenyeji wa eneo hilo kuhama na kuwa katika mazingira hatari. Kila wakati ziwa linapopungua ,wanawake wanalazimika kutembea kwa muda mrefu kutafuta makazi mapya. Wakati wa kiangazi wanaume wanaenda mjini na kuwaacha wanawake vijijini kuangalia jumuiya. Hivyo wanawake wanalazimikia kufanya kazi zaidi ili kutunza watoto bila msaada wowote. Lakini sio wanawake wa maeneo ya vijijini peke yake ndio wanaathirika. Duniani kote wanawake wanaathirika zaidi kutokana na umaskini na kutokuwa na uwezo mkubwa zaidi ya wanaume katika masuala ya kiuchumi hivyo hali ambayo huwafanya washindwe kujikwamua kutoka katika majanga ambayo yanaharibu miundombinu, mazingira, ajira na makazi yao.

Project yetu hii inajihusisha zaidi na jamii ikiwemo kutengeneza uelewa haswa kuwa lenga wanawake, vijana na watoto wakiwa mashuleni juu ya uhifadhi wa mazingira na upandaji miti. Sebastian Chuwa alikua mwana mazingira tangu utotoni kwasababu alikua na baba mwenye uerevu wa kupenda uhifadhi wa misitu kwaajili ya dawa na mengineyo ila pia amerithisha jamii yake inayomzunguka moja kwa moja, vivyo hivyo Sebastian Chuwa amerithisha jamii yake ikianzia kwa mke na watoto na jamii kwa ujumla juu ya mazingira. Leo hii mke wake akitumika kama chambo na mfano wakukuza watoto wake, mashuleni na hata jamii kwa ujumla. Waswahili husema ukimwelimisha mwana-mke ume elimisha jamii hakika hawakukosea kwani katika jamii yetu tunajionea ushawishi mkubwa wa mama zetu.