info@abcpswahili.co.tz
(+255)712 029 665

Wahusika

African blackwood conservation project (ABCP) ilianzishwa 1996 ikiwa na lengo la kuurudisha mti ulioko hatarini kutoweka katika uso wa dunia (Dalbergia melanoxylon) nchini Tanzania, ambapo nimiongoni mwa nchi iliyo na rasilimali nyingi zitokonazo na miti toka 1930, laikni toka kipindi hicho miti na misitu mingi imetoweka kwasababu ya matumizi mabaya ya rasilimali hii kupitia uvunaji haramu wa misitu na upanuzi wa maeneo ya makazi na mashamba bila utaratibu maalum. Mti wa Mpingo ni mti wa kitaifa wa Tanzania, ambao unafaida kubwa sana kiikolojia katika mazingira yetu Afrika mashariki na ulimwenguni, mti huu unafahamika kwa lugha ya kiswahili kama Mpingo..

Project yetu inajihusisha zaidi na jamii ikiwemo kutengeneza uelewa haswa kwa watoto wakiwa mashuleni juu ya uhifadhi wa mazingira na upandaji miti. Sebastian Chuwa alikua mwana mazingira tangu utotoni kwasababu alikua na baba mwenye uerevu wa kupenda uhifadhi wa misitu kwaajili ya dawa na mengineyo ila pia amerithisha watoto wake moja kwa moja.