info@abcpswahili.co.tz
(+255)712 029 665

Shughuli zetu

Je Wajua nini kuhusu mti huu?

International Union for the Conservation of Nature/World Conservation Monitoring Centre(IUCN) katika mwaka 1998 shirika la dunia la kulinda maliasili katika orodha ya mti iliyoko hatarini kutoweka katika uso wa dunia walitaja mti wa Mpingo. Mti wa mpingo ilikuwa nimiongoni mwa aina ya miti inayopatikana kwenye makazi ya mapori katika nchi zilizopo chini ya ukanda wa jangwa la Sahara. Mbao yake hutumika sana katika viwanda vya uchongaji na viwanda kutengeneza vifaa vya ala za muziki.Hatua za utafiti ziko juu sana na kwa kiasi kikubwa, na zinaonyesha aina za mali asili zinazo tumika sana ziko hatarini kutoweka kwenye uso wa dunia. Lakin pia kuna aina nyingi za viumbe vinavyo potea katika jamii nyingi za viumbe duniani. Sebastian Chuwa, Kutokona na utafiti wake ameanisha aina tofauti za viumbe vlivyopo hatarini kutoweka kwenye uso wa dunia kutokana na uharibifu wa mazingira na makazi yao. Kutokana na tafiti hizi Sebastian Chuwa anaamini ni lazima hatua za haraka zichukuliwe juu ya mti wa Mpingo kabla ya siku moja tutakapo amka na kukuta mti wa Mpingo uliopo hatarini umetoweka katika uso wa dunia kabisa, na dunia haikufanya kitu.
Lakini kwanini tujali? Ni swali zuri la kuujiuliza. Leo dunia imetengeneza mazingira ya utegemezi wa mahitaji kutokana na muda wetu na nguvu ya uzalishaji. Lakini utajiuliza maswali, kwanini utusaidie sisi na je, Mpingo una umuhimu gani kati ya vitu vingi vikukubwa? Tutakwenda kutoa majibu ya kitaalamu kulingana na mtazamo wetu. Dunia na mazingira yake chini ya mashambulio kutoka kila pande, mara nyingine inakuwa ni vigumu kujibu mashambulio hayo. Mradi huu unapendekeza kutoa majibu ya moja kwa moja pale unapotakiwa msaada. Ni hatua ndogo ya kutoa suluhisho juu ya matatizo makubwa, lakini safari ndefu inaanza kupitia hatua ndogo. Kwa kupitia kutoa msaada wa moja kwa moja, kwa kuwezesha kutokea ngazi ya chini tunaweza japo tukiwa ni wachache, mazingira ya sehemu nyingi duniani tunaweza kuyabadilisha kutokana na uharibifu, na kuuzuia kutoweka kwa bionuwari ya viumbe na makazi yao ulimwenguni ambavyo vimekuwa vimeharibiwa kutokana na ukuaji wa sayansi na tekinolojia kutokea karne zilizo pita.

Kwanini yatupasa kujali?

“kama miti mikubwa yote inakatwa kwaajili ya mbao, na midogo inakuafa kwa moto, hivyo basi ni dhahiri kuwa hakutokuwa na mipingo yeyote itakayo baki!”

— Sebastian M. Chuwa, "The Tree of Music", 1992 —
about

African blackwood conservation project ni mradi kama ulivo elezewa kwenye vipengele vingine kazi yake kubwa haswa nikutaka kurudisha sehemu ya asili ya dunia iliyo haribiwa kuwa na uhai tena na pia kuwa na mungano kati ya kutunza na matumizi ya mali asili. Mpingo umempa mwanadamu uzuri na heshima katika maisha yake kupitia muziki unao toka kwenye vyombo vya muziki. Kutokana na uwezo wa kuuzuia unyevu, uwezo wa kufanya kazi, uwezo wa kudumu kwa muda mrefu na uimara, vyote hivi vimeufanya mti wa Mpingo kuwa na maana kubwa sana. Kupitia sababu hii tayari inaonyesha umuhimu wa kuutunza mti huu.
Kwa kuongezea, unauwezo pia waku wezesha udongo kujitengenezea madini pamoja na fungi (fungasi) ambao huongeza virutubisho kwenye udongo na pia ni aina moja wapo ya chakula kinacho pendwa na wanyama pori kama Tembo, Twiga na Nyumbu ambapo hupatikana sana makazi ya porini ambayo ipo katika ekolojia ipatikanayo Afrika mashariki. Kupitia wanadamu ongezeko la kiuchumi linapelekea kuongeza sehemu ya ardhi, kuhifadhi baadhi ya maeneo kama sehemu za akiba kwaajili ya kutunza mazingira yetu, mti wa Mpingo una umuhimu mkubwa sana katika maeneo ya mapori na kupitia uvunaji maalum na upandaji kupitia mradi huu inawezekana kufanya yote kwa pamoja.
Kama tukiendelea kutumia rasilimali tulizonazo bila kuangalia mbeleni madhara yake yatakuaje? hii itapelekea ongezeko la bionuwari kuwahatarini kutoweka kwenye uso wa dunia na sisi pia tutapungua kutokana na kutoweka kwao. Kama tunaweza kuweka nguvu kwaajili ya kupata usawa kati ya matumizi na utunzaji wa rasili mali, tutaweza kuishi katika dunia hii kwa vizazi na vizazi na kubaki kuwa na rasili mali nyingi ambazo tumewachia kama urithi.