info@abcpswahili.co.tz
(+255)712 029 665

Mti wa Mpingo

img
Mkato wa mti wa mpingo kwa upande. 90Days

Mpingo (Dalbergia Melanoxylon)

Je wajua mpingo ni mti pekee unaotegemea Carbon Dioxide katika ukuaji!

Mti wa mpingo unaonekana kupendwa pia mwonekano wake mzuri wa weusi uliopo ndani ya kiini chake,lakini pia una rangi mwelekeo mpaka kwenye dhambarau mpauko. Pia ni mti unaosifika kuwa mti bora wa mbao ngumu duniani wenye mn'gao mzuri wa kuvutia. Ubora wa mbao yake inaweza kugharimu mpaka dola za kimarekani 20,000$ kwa robo mita, mara mbili ya mti wa mitiki na Mahogany. Pia huu ni mti mgumu na wakipekee sana kwa wakika wake. Mgumu sana, kiasi hata cha kuvunja shoka wakati wakukatwa, pia hutumika kwa kupikia majumbani kama kuni na pia huachwa kama nguzo za wakika. Ni miti migumu sana kiasi cha misumeno kushindwa kuikata, na hata wakati wakugonga misumari yakupasa kutoboa kwanza.


Mpingo unachukuliwa kuwa "Mti mzuri zaidi ya miti yote ya vifaa vya kutengenezwa, hukatwa nakutengeza vifaa vyenye sura nzuri na rangi ya kupendeza.

Kuna visababishi wakadha kuwa huu mti kushindwa kutengeneza kiini cheusi ndani yake. Mti wa mpingo uliopo jirani na fukwe za bahari kuna hati hati yakuwa na rangi kahawia kwenye kiini chake, hii ni kuonyesha kuwa viduara vya ukuaji wake nivyepesi sana. Pia muda mwingine kwa mpingo wa aina hii huitwa mipingo mieupe au "white mpingo". Kiini cheusi kinasadikika kukua kama mti wa mpingo utakua taratibu sana. Watumiaji wamekuta sana hali hii kuwa kiini kimeamia kwenye ukanda wanje ya mti huu baada ya magamba yake.
Kiini chake kimezungukwa na ukanda wa rangi maziwa kwa inchi 2sm unenewake, hata hivyo kwa majina yake kwa rangi ya punda milia, ukanda wake wa njee ni mwepesi zaidi kuliko ndani kama gram 1.3 kwa senti mita na huzama ndani ya maji. Ukanda wa nje ya ni muhimu kwani huzuia sana wadudu kwa mchwa na fangasi kuharibu mti. Kulinganisha, kiini kina uwezo wakuzuia viumbe hai na mifuu kuoza, hatakama wadudu kama watoboa miti kama bettles wanajulikana kama wenye uwezo wa kuitoboa. baada ya mti kufa kiini cha ndani huisha kwa kipindi cha muda wa miaka mingi sana.

Jina ligine la mpingo

Kwasababu ya weusi wa kiini chake mpingo imekua ikifaamika kama ebony, na mpingo, na mpingo imekua ikifaamika kwa jina la ebony ikitumika na wa Egypt zamani. Pia Mipingo ina mahusiano kidogo na ile ebonies ya kweli ya familia Ebenaceae, na ni kwamba inapatikana rosewood genus, Dalbergia, kwenye familia ya pea.