info@abcpswahili.co.tz
(+255)712 029 665

Wahusika

Kitalu cha Kibosho Mashariki

Katika historia ya Kibosho, wazee wanatueleza kwamba tangu kupata uhuru kuanzia mwaka 1961, kaya zilikuwa chache, na wazee walikuwa wakifaidika sana na zao la kahawa, pia walikuwa na nafasi kulima na kuchungia mifugo katika msitu ya hifadhi ya mlima kilimanjaro, na baada ya ujamaa, kwenye eneo la Chibo. Ukame wa njaa ulilitokea kila miaka kumi. Kuanzia kipindi cha vita vya Kagera mwaka wa 1978, hali imebadilika. Bei ya kahawa ilishuka kwenye soko la dunia, sera ya uchumi na kilimo ilibadilika kuondoa ruzuku na mikopo na kupanda bei ya kilimo hasa madawa ya kahawa. Vilevile sheria ya msitu wa Kilimanjaro zilianza kuzuia matumizi ya msitu hadi yakachukuliwa na Hifadhi ya Kilimanjaro kusabibishwa na uharabifu wa msitu.

Mwaka 1996, jamii na vikundi vya mzaingira mbalimbali kutoka Kibosho mashariki na vile vilivyopo jirani na mlima mkoani Kilimanjaro Tanzania, kwasababu ya uthubutu wao na utayari walionao juu ya utunzaji wa mazingira, walipewa na kuchaguliwa kuwa mkoa pekee utakao fanya sherehe za mazingira kwa mara yakwanza mkoani hapo. Kwa ushiriki mkubwa kutoka UN (Umoja wa matifa) walifanikisha kufanya sherehe za siku za mazingira duniani, iliofanyika mwezi juni 5. Na hii imefanya siku hiyo kuwa sikuu pekee ya mazingira ambapo kila mwaka huadhimishwa nakufatwa kitaifa. Pia kwa siku hiyo mashule na vikundi mbalimbali vya mazingira, klabu za mazingira, kwaya na jamii pamoja na viongozi wa serikali.

Sebastian Chuwa alitumika kama chombo cha kuunganisha jamii na wanafunzi mashuleni na vikundi mbalimbali katika jamii waliochaguliwa kushiriki katika matamasha haya ya mazingira, pia akiwa kama msimamizi na baba mlezi wa makundi yote haya mazingira kilimanjaro alikua wa kwanza katika kuamsha matukio haya ya mazingira . Kwa kushiriki wa wanfaunzi, Waalimu, na wengine waliojitolea katika jamii kwa msaada mkubwa kutoka Rafiki/Friends Foundation huko California, USA(Marekani), a kiungo kitabu kilitengenezwa. Kitabu hiki pekee kiliweza kuzalisha kurasa na kueleza juu ya matukio makuwa katika sherehe za mazingira pia kilitoa taarifa muhimu za utunzaji wa mazingira na ushauri. Mfano wa kitabu hiki unapatkana kwa kurasa chache ambapo hakija pata chapisho lilokamilika tangu kutengeneza kwake ila ABCP, tunatoa kitabu hiki kwa mfano wake katika tovuti yetu hii ya kipekee.

Kitabu kina matukio muhimu ya mazingira kutoka kibosho mashariki kwa namna yanavyo tokea mara kwa mara, na taarifa zake juu ya uhifadhi wa mazingira hazina mwisho. Pia kina toa taarifa muhimu juu ya sebastaian Chuwa juu ya juhudi zake kuwa ratibu waalimu na wanafunzi juu ya mambo muhimu juu ya campaign za uteshaji wa miti, (zaidi ya miti milioni moja imeoteshwa tiyari !), na pia kuwajengea jamii uwezo wakujitambua kuhusu mazingira ya wazungukayo na utunzaji wake. Pia muhimu kuliko vyote moja wapo kati ya kurasa za kitabu hiki muhimu ni list ya miti iliopo chini ya mlima kilimanjaro, ndege, aina ya wanyama wapatikanao, miti asilia kwa matumizi ya dawa Pia kuna picha za kuvutia nzuri sana zenye rangi.

Chapisho hili linapatikana kwa lugha ya kiingereza kwa mfumo wa .pdf (Adobe Acrobat PDF format), na program ya bure kabisa Adobe Reader ambayo ni lazima kwaajili yakufungulia kitabu hiki. Chapisho hili linapatikana katika tovuti yetu ya lugha ya kiingereza Bofya hapa kusoma nakala hii.