info@abcpswahili.co.tz
(+255)712 029 665
img

VIJANA

Shule ya Sekondari ya wasichana Mt. Theressa wa Avila wamekuwa wakifanya kazi na ABCP tangu mwaka 2015, wakilenga sana katika upandaji wa miche ya mpingo kwenye mashamba yao ya shule. Lengo kuu kuwajenga vijana wakike haswa katika taaluma, mazingira na uongozi.

Soma zaidi
img

KIBOSHO MASHARIKI

Jamii kutoka kibosho mashariki walikubali kupeleka mazingira mbele ili kuboresha mazingira na hali ya kiuchumi, wewe je?

Soma zaidi
img

MPINGO

Cyril na Marie-Justine(Mwandishi kutoka ufaransa) wakiwa na mahojiano juu ya mti wa mpingo katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Soma zaidi
img

ELIMU

Umaskini na uharibifu wa mazingira ni watoto mapacha na mama yao ni ujinga Mhe. (Ali Hassan Mwinyi 1998).Jamii huwa haitambuliki bila kumtaja mwanamke, jamii bora ni ile inayo pata maono ya kesho....

Soma zaidi

ELIMU

Mwanadamu anapaswa kupata taaluma na ujuzi utakaomsaidia kufahamu na kuenzi mazingira yake, kujifunza kuna manufaa.

UBUNIFU

Usafi wa mazingira ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia mawasiliano ya binadamu na athari za taka.

MAZINGIRA

Mazingira ni vitu vyote vinavyotunzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama.

AFRICAN BLACKWOOD CONSERVATION PROJECT(MPINGO)

African blackwood conservation project (ABCP) ilianzishwa 1996 ikiwa na lengo la kuurudisha mti ulioko hatarini kutoweka katika uso wa dunia (Dalbergia melanoxylon) nchini Tanzania , ambapo nimiongoni mwa nchi iliyo na rasilimali nyingi zitokanazo na miti tangu 1930, lakini toka kipindi hicho miti na misitu mingi imetoweka kwasababu ya matumizi mabaya ya rasilimali hii kupitia uvunaji haramu wa misitu na upanuzi wa maeneo ya makazi na mashamba bila utaratibu maalumu. Mti wa mpingo ni mti wa kitaifa wa Tanzania, ambao unafaida kubwa sana kiikolojia katika mazingira yetu Afrika mashariki na ulimwenguni, mti huu unafahamika kwa lugha ya kiswahili kama mpingo..

“kama miti mikubwa yote inakatwa kwaajili ya mbao, na midogo inakuafa kwa moto, hivyo basi ni dhahiri kuwa hakutokuwa na mipingo yeyote itakayo baki!”

— Sebastian M. Chuwa, "The Tree of Music", 1992 —

Je Wajua nini kuhusu mti huu?

about about about about

Watu wengi hawaufahamu au kuuona mti wa huu, lakini unasikika sana kwa watu wengi kutokana na faida za kazi yake, kulingana na ubora wake unatumika kutengeneza vifaa mbalimbali vya muziki kama vile filimbi (clarinets, oboes, flutes and bag pipes) gitaa na vinanda kutokana na uwezo mkubwa wa mti huu kufanya vifaa hivi vya muziki kuweza kutoa ala za muziki na kuweza kutumika katika utunzi wa sanaa mbalimbali. Kipindi cha miaka ya 1800 aina moja ya mti wa kutoka mataifa ya magharibi uitwao cocuswood ulikuwa ukitumika sana kama mti wa kutengeneza vyombo vya muziki lakini punde ukawa mti wa biashara na ukatoweka kabisa kwenye uso wa dunia na ndipo ulipo gundulika mti wa mpingo kama mti wa kutengeneza vifaa vya muziki.

Mpingo hadi leo unasifa kubwa sana kutokana na uwezo mkubwa na ubora zaidi katika kutengeneza vifaa vya muziki na uchongaji wa vinyago, ambapo nchi za bara la marekani na ulaya limetoa soko la ajira kwa wana sanaa wa mabara hayo. Lakini kwa Afrika umekuwa ukitumika kwa matumizi makubwa ya uchongaji wa vinyago ambapo uchongaji huo unaakisi maisha halisi, tamaduni za watu wanao tumia mti huo. Katika nchi ya Kenya kabila la wa Kamba na wa Makonde wa nchini Tanzania wamekuwa na sifaa kubwa ya uchongaji wa vinyago ambapo wamerithishwa kutoka kwa mababu na wajukuu wao kupitia vizazi vingi. Kupitia biashara ya utalii Afrika mashariki imefungua soko kubwa la biashara ya kuuza vinyago vyao, matokeo yake ni katika ongezeko la uhitaji na uvunaji haramu wa mti wa mpingo, ambapo wachonga vinyago wanalazimika kutafuta aina nyingine ya mti utakao weza kuwezesha kazi yao na kumudu tamaduni na maisha yao halisi kutokana na upungufu na kutoweka kwa mti wa Mpingo. Kujua zaidi kuhusu mti wa mpingo bofya hapa.

Baadhi ya matukio

African Blackwood Conservation Project.

img
ABCP

Elimu

ABCP tumepata fursa ya kutembelewa na mgeni kutoka Zambia Dr. Nyuma(Daktari wa magonjwa ya ukanda wa kati), alikuja kwa nia ya kujifunza mambo mbalimbali hususani ukuwaji wa mti hu wa mpingo na faida zake

img
Sungu Primary

Elizabeth mwl. Mashuhuri

Kwa takribani miaka 37 sasa Elizabeth anawafundisha watoto umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kusaidia jamii yake katika utunzaji wa miti kwa kufundisha kwa vitendo na ueledi......

img
Dar es salaam

Marie Justine na Cyril Chuwa

Cyril akihojiwa na Marie-Justine Fournier, nchini Tanzania kutoka "France-Canadian Television" wakati alivyo tembelea soko la wachonga vinyago wa Kimakonde, walijadili malengo na shughuli za ABCP kuelekea uhifadhi wa mpingo.

img
Maadhimisho ya Siku ya mazingira

Sikukuu ya Mazingira

Pichani ni mgeni rasmi ndugu Dismas Macha (mtaalamu misitu na uhifadhi NCAA)akitunuku vyeti vya mazingira kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani Same mkoanis wa Moshi-Kilimanjaro.

“kama miti mikubwa yote inakatwa kwaajili ya mbao, na midogo inakuafa kwa moto, hivyo basi ni dhahiri kuwa hakutokuwa na mipingo yeyote itakayo baki!”

— Sebastian M. Chuwa, "The Tree of Music", 1992 —